Ku-move pesa. Ku-power biashara. Selcom Inatosha!

  • 1B+

    Miamala iliyowezeshwa

  • 500K+

    Biashara zilizounganishwa

  • 20M+

    Wateja waliohudumiwa

  • 20+

    Miaka ya kuihudumia Africa

Kwa ajili ya Africa

#SelcomInatosha

Safari yetu Ilianza 2001

Selcom ilianza mwaka 2001 kama msambazaji wa muda wa maongezi wa kulipia kabla (prepaid airtime) wa Celtel jijini Dar es Salaam. Kilichoanza kama biashara ya usambazaji kiligeuka haraka kuwa fursa ya kutatua changamoto kubwa zaidi: Jinsi ya kufanya huduma za kifedha zipatikane kwa urahisi zaidi, ziunganishwe na ziwe rahisi kutumia.

Kutokana na hapo, Selcom ilianza kujenga teknolojia na mitandao iliyowaunganisha watumiaji, wafanyabiashara, benki na taasisi mbalimbali. Kama mfumo wa huduma za kifedha na teknolojia unaopanuka barani Afrika, kwa zaidi ya miongo miwili Selcom imekuwa ikijenga miundombinu inayowasaidia watu, biashara na taasisi kutuma na kupokea fedha, kufanya malipo, kuunganishwa na kukua. Leo, Selcom inaunganisha huduma za malipo, benki, biashara na teknolojia za kifedha, ikiwawezesha watu na biashara kunufaika na fursa zinazotokana na uchumi wa kidijitali unaoendelea kukua.

Kutoka malipo mpaka system nzima ya kifedha

Kwa miaka mingi, Selcom imeendelea kutoka kuwa kampuni ya miundombinu ya malipo na kuwa mfumo mpana wa huduma za kifedha na teknolojia.

Leo, uwezo wetu unajumuisha malipo ya kidijitali, huduma za benki, huduma za malipo kwa wafanyabiashara (merchant acquiring), huduma za kibenki kupitia mawakala, kadi na uchakataji wa malipo, makusanyo ya bili na malipo ya serikali, biashara mtandaoni, huduma za benki kwa biashara, huduma za kifedha za kidijitali, API za malipo na teknolojia.

Mfumo wetu unaunganisha benki 40+, mawakala 50,000+ na wafanyabiashara 200,000+, na kuwezesha shughuli za kiuchumi zenye thamani ya mabilioni.

Kuisuka benki yetu

Hatua muhimu katika safari ya maendeleo ya Selcom ilikuwa ni kuunganishwa kwa Access Microfinance Bank katika familia ya Selcom. Taasisi hiyo baadaye ilibadilishwa jina na kuwa Selcom Microfinance Bank, na hivyo kuleta uwezo wa huduma za benki zinazodhibitiwa kisheria ndani ya mfumo mpana wa Selcom.

Hili liliifanya Selcom kuwa zaidi ya kampuni ya huduma za malipo. Liliipa Selcom uwezo wa kuunganisha malipo, huduma za benki, teknolojia na biashara katika mfumo mmoja.

Leo, Selcom Microfinance Bank ndiyo msingi wa huduma za benki unaodhibitiwa kisheria unaowezesha bidhaa kama Selcom Pesa na Selcom Business.

Selcom Paytech hutoa suluhisho zinazojumuisha upokeaji wa malipo, huduma za kibenki kupitia mawakala, utoaji wa kadi, huduma za kutuma na kupokea fedha, makusanyo ya mapato na biashara mtandaoni. Kwa kuzingatia ubunifu, muunganisho na ujumuishaji wa huduma za kifedha, Selcom Paytech inaendelea kujenga teknolojia na miundombinu inayowezesha watu na biashara kupata na kutumia huduma za kifedha kwa urahisi zaidi.

Selcom Microfinance Bank imepewa leseni na kusimamiwa na Benki Kuu ya Tanzania (Bank of Tanzania) na ndiyo kiini cha huduma za watumiaji na biashara ndani ya makampuni ya Selcom.

Kinachoitofautisha Selcom

Tunaunganisha kila sehemu. Hatuamini kwamba huduma za kifedha zinapaswa kufanya kazi kwa kutengana. Tunaunganisha watu + biashara + benki + wafanyabiashara + teknolojia katika mfumo mmoja unaozidi kuunganishwa na kufanya kazi kwa pamoja.

Ubunifu.
Kujenga teknolojia hapa nchini ili kutatua changamoto halisi za Afrika.

Upatikanaji.
Huduma za kifedha zilizo karibu na nafuu zaidi kupitia njia za moja kwa moja na za kidijitali.

Muunganisho.
Kuunganisha benki, huduma za kidijitali, kadi, wafanyabiashara na taasisi.

Uaminifu.
Kufanya kazi ndani ya mifumo ya huduma za kifedha na malipo inayodhibitiwa kisheria.

“Tunawekeza katika teknolojia ya kifedha ili kufanya huduma za kifedha ziwe nafuu zaidi, si kuwa ghali zaidi. Teknolojia inapaswa kushusha gharama, kuongeza upatikanaji na kuleta thamani karibu zaidi na watu.”

Misingi yetu

Selcom, jina letu ni zaidi ya chapa—linaakisi sisi ni nani na namna tunavyofanya kazi. Kila herufi katika SELCOM inawakilisha thamani ya msingi inayowaongoza watu wetu, maamuzi yetu na namna tunavyotengeneza matokeo chanya.

S – Speed, E – Elekea, L – Leadership, C – Clarity, O – Ownership, and M – Moyoni. Pamoja, misingi hii inaifanya Selcom iende kwa malengo

Speed

Tunatekeleza.
Tunachukua hatua kwa haraka na kutekeleza kwa uhakika.

Clarity

Keep it clear.
We communicate openly, simply and often.

Elekea

Tunasonga mbele pamoja.
Tunasonga mbele kwa bidii, ari na mshikamano wa timu.

Ownership

Weka wazi.
Tunawasiliana kwa uwazi, kwa urahisi na mara kwa mara.

Leadership

Ongoza njia.
Tunaunganisha, tunabuni na tunaunda suluhisho za kesho.

Moyoni

Kutoka moyoni.
Tunawaheshimu, kuwajali na kuwaweka watu katikati ya kila tunachofanya.

Sura inayofuata ya Selcom inahusu kwenda zaidi ya miamala. Tunajenga mfumo uliounganishwa ambapo huduma za benki, malipo, biashara na teknolojia vinafanya kazi pamoja kwa urahisi na ufanisi. Tunaiona kesho ambayo...

Tunajenga miundombinu ya kifedha ya kesho.

Zungumza na Selcom